Breaking News

RAIS SAMIA MGENI RASMI MKUTANO WA WADAU WA DEMOKRASIA YA VYAMA VYA SIASA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe Samia Suluhu Hasani anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wadau wa vyama vingi vya vyama vya siasa  utakaofanyika Desemba 16 - 17 mwezi huu jijini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya Siasa nchini, mhe. Juma Ali Khatibu amesema mkutano utakao waleta pamoja wadau wa vyama vya siasa, viongozi wa dini na wadau wengine kubadilishana mawazo kujadili kuzipatia ufumbuzi changamoto zilizopo.

Kabla ya kuanza kwa mkutano utatanguliwa na seminna ya siku moja desemba 15 kwa wajumbe wa baraza la vyama vya siasa ambao utahusu historia na majukumu ya baraza hilo.

"Tukiwa tunaelekea kuadhinisha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania bara, baraza la vyama vya siasa nchini tunakutana kujadiliana ma kubadilishana mawazo na uzoefu juu hali ya demokrasia nchini". Alisema mhe. Khatibu

Mhe. Khatibu ameongeza kikao hicho wajumbe wa kikao hicho wapatata wapata wasaa wa kujadiliana na kuwezesha kuweka sheria zinazoratibu shughuli za vyama vya siasa, kuboresha na mazingira hili kuviwezesha vyama hivyo kufanya shughuli zake kwa uhuru unaohitajika.

Nae Mwenyekiti wa chama cha UDP, Mzee John cheyo amewataka viongozi wa vyama vya siasa nchini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mkutano huo kwani ni moja ya fursa kwao kuweza kutoa na kuwasilisha changamoto mbalimbali na zikapatiwa ufumbuzi.

"Nitoe wito kwa viongozi wa vyama vya siasa nchini kujitokeza kwa kwa wingi siku ya tukio hili kuweza kutoa na kuchangia juu ya mbo mbalimbali yanayowasibu tamgu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi hili zijadiliwe na kupatiwa ufumbuzi"

Nae Mwenyekiti wa kamati ya Maadili ya Baraza la vyama vya Siasa nchini, Mhe. Doyo Hasani Doyo amesema kikao hicho muhimu kwa vyama vya siasa nchini kuelekea maadhimisho ya miaka 60 tangu uhuru wa Tanzania hivyo niwaombe wadau wote kushiriki hili kuweza kujadili na kupata muhafaka wa chamgamoto zote wanazolutana nazo.

"Kikao hiki ni muhimu sana kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru hivyo kitasaidia kuwezesha kutambua changamoto zilizopo pamoja na kudumusha umoja na mshikamano ka taifa". Amesema mhe. Doyo .

No comments