Breaking News

RAIS SAMIA AMETOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 5,704

Timothy Marko
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan ametoa msamaha kwa wafungwa 5,704 ambao walikuwa wakitumikia vifungo katika magereza mbalimbali nchini.

Akizungumza jijini Dar es salaam Waziri wa Mambo ya ndani mhe. George Simbachawene amesema wanufaika wa msamaha huo ni wafungwa ambao ni wagonjwa na wamethibitishwa na madaktali chini na mganga mkuu wa Mkoa au wilaya.

"Kwa mujibu ibara ya 45(1)(d) ya katiba ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan ametoa Msamaha wafungwa 5,704 ". alisema Simbachawene.

Waziri Simbachawene aliongeza kuwa msamaha huo utawahusu wafungwa wenye umri miaka 70 au zaidi na uliothibitishwa na Mganga Mkuu.

Alisema pia msamaha huo utawahusu wafungwa wa kike waliongia na mimba Gerezani pamoja na wale walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya.

"Wafungwa wenye Ulemavu wa Mwili na akili na na uliothibititishwa na jopo la madaktari nchini". Aliongeza

Katika hatua nyingine Waziri huyo Alisisitiza msamaha huo wa Rais hautawahusisha wafungwa wanaotumikia adhabu ya kunyongwa na wenye makosa  ya kujaribu kuua aubkujiua sambamba na kuua watoto wachanga.

Alisema pia wafungwa wanaotumikia kifungo chini ya sheria ya bodi ya Parole (act.No 6/2002 na kifungo cha nje.

No comments