Breaking News

JESHI LA POLISI KANDA MAALUM DAR YATANGAZA MATOKEO YA OPARASHENI KUBWA INAYOENDELEA

Timothy Marko
Jeshi polisi kanda maalum ya Dar es salam linamshikilia mtu mmoja jina lake limehifadhiwa mkazi wa Gerezani Kwa tuhuma za kukutwa na gunia la bangi lenye uzito kilogram 35.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Kamanda wa kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP Muriro Jumanne Muliro amesema mtuhumiwa huyo anatarajia kufikishwa Mahakamani, sambamba na hilo pia jeshi Hilo limekamata Gari Aina ya Toyota Aina wish yenye usajili T 489 DBZ pamoja na pikipiki nne Aina  Boxer zenye namba za usajili MC 693 CLH, T 128 CMY, MC 649 na MC 455 CWD huku zote zikiwa na Rangi nyeusi.

"Pipiki hizi zimeibiwa katika Maeneo tofauti sambamba na wezi wa pikipiki hizo pia tumefanikiwa kukamata Television 15 ambazo zimepatikana Kwa wizi". Alisema Kamanda ACP Muliro.
Alisema sambamba na Mali hizo za wizi pia jeshi Hilo linashilia Friji  pamoja na vifaa vya tarikishi sambamba komputa mpakato ambazo zimeibiwa na watuhumiwa 26 katika Maeneo mbalimbali jiji.

Katika hatua nyingine Jeshi limejipanga kuhakikisha kuna kuwa na utulivu kuelekea sikukuu ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara kwa kuanza kuendesha operesheni Kali dhidi ya uhalifu.
"Natoa onyo atakaye jihusisha, kuratibu na kupanga kuandaa vya kihalifu atashughulikiwa zaidi pia nitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi mapema pindi watakapo ona kuwepo viashiria vya uvunjifu wa amani pamoja na matukio ya uhalifu  ".Aliongeza Muliro

No comments