Breaking News

DED LUBWA: WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA AMASISHENI WANANCHI KUCHUKUA TAADHALI NA KUPATA CHANZO YA UVIKO 19

Na Timothy Marko
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam mhe. Hassan Lubwa amewataka watendaji wa Serikali za Mitaa kuendelea kuwahimiza wananchi kuchukua taadhali pamoja na kujitokeza kuchanja chanjo ya Uviko 19 katika Maeneo Yao.

Wito huo ametolewa jijini Dar es salaam wakati akifungua mkutano ulio wakutanisha watendaji wa Serikali za Mitaa kujadiliana  na juu ya namna wanavyoweza kutumia nafasi zao Kuhamasisha wananchi wanajitokeza kwa wingi kuchanja chanjo hiyo.

"Lazima kila mmoja katika Maeneo yenu kubainisha ni watu wangapi wamechanja na watu wangapi hawaja chanjwa na kwasabu gani awaja chanja". Alisema mhe. Lubwa

Alisema wenyeviti mnao wajibu wa kuhamasisha jamii kuwa Salama na janga la uviko 19 ikiwemo usimamizi wa hatua zote ikiwemo uvaaji wa barakoa.

Kwa upande wake Mwakilishi wa wenyeviti wa Serikali za Mitaa Bw. Juma Abbass amesema wenyeviti wa serikali za Mitaa wanayo nafasi kubwa katika kufikisha ujumbe ngazi ya mtaa juu ya chanjo hiyo ya Uviko19.

"Tunaahidi kutekeleza majukumu na wajobu wetu kwa kadri itakavyo elekezwa na tukuhaidi kuwa tutafikia malengo yaliyokusudiwa". Alisema Bw. Abbass.

No comments