MAJINA YA WAGOMBEA NAFASI YA MWENYEKITI TAIFA WA CHAMA CHA WANANCHI CUF
Wagombea Uenyekiti Taifa:
|
||||||||
NO.
|
JINA
KAMILI
|
UMRI
|
JINSIA
|
ELIMU
|
MAFUNZO
YA KITAALAM
|
|||
1
|
Abdul
Omari Zowo
|
66
|
ME
|
Secondari
|
Enginearing
ndege za Kivita China na Urusi
|
|||
2
|
James
Kija Mahangi
|
42
|
ME
|
Sekondari
|
Upimaji
wa magonjwa ya Binaadamu (MAABARA)
|
|||
3
|
Joseph
Magoiga Rhobi
|
48
|
ME
|
-
|
Ufundi
Seremala
|
|||
4
|
Juma
Shabani Nkumbi
|
49
|
ME
|
Secondari
|
Computer
Course
|
|||
5
|
Riziki
Shahari Mngwali
|
56
|
KE
|
Chuo
kikuu
|
Usuluhishi
wa Migogoro
|
|||
6
|
Salum
Khalfan Barwany
|
57
|
ME
|
sekondari
|
Ufundi
Magari
|
|||
7
|
Selemani
Khatibu
|
37
|
ME
|
Sekondari
|
|
|||
8
|
Twaha
Issa Taslima
|
63
|
ME
|
Chuo Kikuu
|
Sheria
|
|||
9
|
Zuberi
Mohamed Kuchauka(MB)
|
54
|
ME
|
Chuo
|
F.T.C.
Mechanical
|
|||
Wagombea Makamo Uenyekiti Taifa:
|
||||||||
NO.
|
JINA
KAMILI
|
UMRI
|
JINSIA
|
ELIMU
|
MAFUNZO
YA KITAALAM
|
|||
1
|
Dr.
Juma Amer Muchi
|
|
ME
|
Chuo
Kikuu
|
Afya
|
|||
2
|
Juma
Duni Hajji
|
|
ME
|
Chuo
Kikuu
|
Uchumi
|
|||
3
|
Mussa
Hajji Kombo
|
|
ME
|
Sekondari
|
|
|||
4
|
Salim
Abadalla R. Bimani
|
|
ME
|
Chuo
|
|
Waheshimiwa Waandishi wa habari, kwa niaba ya Chama Cha
Wananchi CUF Juni 2, 2016 CUF kiliitisha
kikao na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Shaaban Khamis Mloo kwa lengo la
kuelezea kuitishwa kwa Mkutano Mkuu wa Chama wa taifa ambao ungetumika kujaza
nafasi mbalimbali za uongozi zilizo wazi.
Tulieleza kwamba nafasi zilizo wazi ni ya Mwenyekiti wa taifa
wa Chama na hii imetokana na aliyekuwa Mwenyekiti wetu Profesa Ibrahim Lipumba
kuamua kujiuzuru mwenyewe katika nafasi hiyo mnamo tarehe 5 August 2015, pia
nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa taifa iliyotokana na Mheshimiwa Juma Duni Haji
kujiuzuru nafasi hiyo na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) ili aweze kuwa mgombea Mwenza wa Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia Chama hicho Mheshimiwa Edward Lowassa aliyeungwa
mkono na vyama vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA.
Nafasi nyingine zilizowazi ni pamoja na nafasi nne za Ujumbe
wa Baraza Kuu la Uongozi la taifa kwa
Kanda zifuatazo, idadi na aina na wajumbe wa kuchaguliwa katika mabano: Nafasi
moja ya mjumbe kutoka Kanda ya Nyanda za juu kusini (Mjumbe yeyote wa Kanda
hiyo anaweza kugombea), nafasi moja ya mjumbe kutoka Kanda ya Kati (Mjumbe
yeyote wa Mkutano Mkuuu taifa kutoka Kanda hiyo anaweza kugombea, nafasi moja
ya mjumbe kutoka Kanda ya Ziwa (ni Mjumbe mwanamke tu kutoka kanda hiyo anaweza
kugombea) na nafasi moja kutoka Kanda ya Kaskazini (mjumbe yeyote kutoka Kanda
hiyo anaweza kugombea.
Katika ratiba ya matukio kuelekea siku ya Mkutano Mkuu maalum
wa taifa tulieleza kwamba uchukuaji wa fomu za kuomba nafasi za kugombea
utafanyika kwa Makatibu wa wilaya na kwamba siku ya mwisho ambayo Makatibu wa
wilaya watapaswa kuwasilisha taarifa za waliogombea pamoja na fomu zao kwa
Katibu Mkuu ni tarehe 10 August 2016.
No comments